Ruka hadi kwenye maudhui makuu

VYOO VYA KUKAA VINAWEZA KUSABABISHA SARATANI

Habari za leo ndugu wasomaji wa blogu ya Sayansi Leo,katika makala hii ya leo tutazungumzia njia sahihi ya kujisaidia haja kubwa. Ndio njia sahihi yakujisaidia haja kubwa,linaweza onekana kua ni swala la ajabu au la utani lakini mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamekuja na madhara pamoja na faida.



matumizi ya vyoo vya kisasa vyakukaa
kielelezo na.1
Kwakuanza tutatazamia juu ya njia ya asili ambayo binadamu anatakiwa kutumia iwapo ataenda haja kubwa..

         Kwa mazoea, jamii nyingi za Afrika watu wake huchuchumaa waendapo haja kubwa. Katika miaka ya hivi karibuni baada ya mapinduzi ya viwanda uko katika nchi za magharibi kumeundwa vyoo vya kukaa. Vyoo hivi vimeonekana kua ni ishara ya maendeleo katika jamii za Wafrika ambao wengi walizoea vyoo vya shimo.. Vyoo hivi sio vyakwanza bali  ni muendelezo wa vyoo vya kigae vyakuchuchumaa vilivoiga mfano wa vyoo vya awali vya asili ambavo pia vilikua vyakuchuchumaa.  vyoo vya vigae vya kuchuchumaa viliboreshwa kwa kuwekewa mfumo wa kujisafisha endapo mtu atamaliza haja,kwa njia zifuatazo kamba itakapovutwa,au kitasa kitakapozungushwa au kitufe kitakapominywa basi maji yangemwagika kwa presha kubwa na kuondoa kinyesi kwenye choo husika na kukisukuma kwenye shimo la choo.

MADHARA YA VYOO VYA KUKAA YANAPATIKANA VIPI?

Mtu anapokaa misuli yake inayoshikiria kihifadhi kinyesi hua
imebana nusu kwahiyo kuzuia tendo la kuondoa kinyesi chote
kama picha ya kwanza inavoonyesha, mtu anapokua amechuchu
maa misuli yake hua inakua imeachia kabisa hivo kuruhusu
kinyesi kutoka kwa wepesi zaidi na kutoka chote.
kielelezo na.2
     Baada ya mmeng'enyo wa chakula chakula upita kwenye utumbo mdogo ambapo ufyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu,chakula ambacho hakipati nafasi ya kufyonzwa uendelea na safari mpaka kwenye utumbo mkubwa ambako uko maji na madini ufyonzwa na kuingizwa kwenye mfumo wa damu, chakula hiki kinachobaki kikiwa na kias kidogo cha maji upelekwa kwenye kihifadhi kinyesi kwa jina la kimombo rectum.. na apo kihifadhi kinyesi kinapojaa basi mtu ujisikia kubanwa na haja.

Hii yote ni bado haijaeleza madhara yanatokea vipi vya matumizi ya vyoo vya kukaa..  na haya ndo majibu ya jinsi gani madhara yanamfika mtu.

Mtu anapokaa kwenye choo njia yake ya kihifaadhi kinyesi hua imebanwa kiasi kwa hiyo hua hatoi kinyesi chote wakati wa kujisadia hali hii uchangiwa kutokujikunja vyakutosha na kuweka presha kwenye mfuko huo.. Kwa hali hii misuli inayoshikiria kihifadhi kinyesi kua imelegezwa nusu tu ya jinsi inavotakiwa iwe imelegezwa. Lakini mtu anapochuchumaa, ukunja eneo hili kwa nyuzi za kutosha kuruhusu misuli (sphincter muscles) hiyo kulegea vya kutosha na kurahisisha kinyesi chote kutoka nje na hivo kukidhi haja nzima, tazama  kielelezo namba 2.


MADHARA YA KUKAA WAKATI WAKUJISAIDIA HAJA KUBWA.




  1. KUPATWA NA UGONJWA WA BAWASIRI : Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na
    nnje ya sehemu ya haja kubwa kutokana na mishipa kubanwa kwa mda mrefu na kinyesi ambacho mara nyingi hua ni matokeo ya kutomaliza haja au kubana kwenda mapema haja madhara yake wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kusababisha kutoka kinyama au uvimbe 
    ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu unaitwa HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles soma zaidi hapa kuhusu bawasiri
  2. SARATANI YA UTUMBO MPANA:  Mtu mwenye bawasiri mara nyingi hua kwenye hatari ya kupatwa na saratani ya utumbo mpana japoa sababu nyingine hua ni kurundikana kwa kinyesi mda mrefu jambo ambalo husababisha kinyesi icho kugeuka sumu na hivo kusababisha madhara kwenye utumbo mpana madhara haya yanaweza kukua mpaka kua saratani endapo hayatatafutiwa tiba haraka.soma zaidi juu ya saratani ya utumbo mkubwa
  3. KUPATA SHIDA YA HAJA NDOGO KWA WANAWAKE:  Maumbile ya mwanamke yameumbwa kufanya kazi vizuri wakati akiwa kwenye mkao wa kuchuchumaa wakati wa haja zote mbii choo cha kukaa uleta madhara yale yale yakukosa kukojoa mkojo wote na hvo inaweza sababisha madhara kwenye kibofu cha mkojo 
  4. KUKOSA CHOO:  Mtu anaetumia choo cha kukaa mara nyingi hua hamalizi haja na mlundikano wa haja ufanya kinyesi kua kigumu na kupelekea mtu kupata choo kigumu atakapojisadia wakati mwingine 
  5. MAGONJWA YA NGOZI:Vyoo vya kukaa huweza kuambukiza magonjwa ya ngozi kwenye makalio endapo vitatumiaka sehemu za umma ambako kusimamia usafi wa vyoo hivyo hua nni kazi ngumu.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HIZI NDIO NJIA BORA ZA KUFANIKIWA KIMASOMO

Je umekua ukisoma sana nyakati za karibia na mitihani na bado matokeo ni finyu ukiringanisha na wakati unaotumia, bila kusahau kukesha usiku kucha? soma zaidi upate siri ya kufanikiwa katika masomo yako katika ngazi tofauti tofauti za elimu ikiwemo elimu ya chuo kikuu. masomo binafsi kwenye eneo tulivu KUSOMA MAANA YAKE NINI? Watu wengi hatujui kusoma maana yake nini,labda hufikiri kusoma ni wakati ule unaposhika daftari au kitabu au kitini kwaajili ya kusomea mtihani ambao unao kesho asubuhi. Lakini watafiti wanasema kusoma hua ni mchakato mpana zaidi ya apo. Kwa kifupi kusoma maana yake hua ni kuandika notsi kwa urefu(kutolea maana kila pointi ulioiandika), kuandika points,bila kusahau kuvisoma hivo ulivoviandika. NAMNA YAKUFANIKIWA KATIKA MCHAKATO WAKUSOMA: TAFUTA ENEO LA KIMYA: inaweza kua chumba tulivu kama hiki ambacho hakina usumbufu kabisa                    Watu wengi usoma popote bila kujali kama en...

NAMNA YA KUTUMIA WI-FI YAKO KUTOKA KWENYE TARAKILISHI (KOMPYUTA)

UTANGULIZI: Habari ndugu wasomaji, leo ntawafundisha namna yakutengeneza Wi-Fi (wireless fidelity) kutoka kwenye tarakilishi mpakato au ya kwenye desk: MAHITAJI: 1.  TARAKILISHI (KOMPYUTA) YA MEZANI(DESKTOP) AU MPAKATO YENYE WIRELESS CARD (KADI YA WIFI) AU YENYE UWEZO WAKUDAKA WIRELESS AU BLUETOOTH 2. UJUZI WA KAWAIDA WA KUTUMIA TARAKILISHI  HATUA YA KWANZA: Unahitajika kua na uwezo wakuunganisha intanet kwenye kompyuta yako kama utatumia modem au utatumia wireless(Wi-Fi) kutoka kwenye eneo ambalo tarakilishi yako imeunganishwa. intanet ya WiFi (kwenye duara jeusi) HATUA YA PILI: Tutatakiwa kushusha (download) Baidu "wifi share app" kutoka kwenye tovuti ya PC FASTER nimekuwekea link hapa uishushe haraka   shusha baidu moja kwa mojahapa    au unaweza tembelea tovuti yako hapa  shusha program yako ya Baidu kwenye tarakilishi yako( kwenye picha ninatumia program ya IDM kushusha BAIDU kwa haraka ) ...