Ruka hadi kwenye maudhui makuu

HIZI NDIO NJIA BORA ZA KUFANIKIWA KIMASOMO

Je umekua ukisoma sana nyakati za karibia na mitihani na bado matokeo ni finyu ukiringanisha na wakati unaotumia, bila kusahau kukesha usiku kucha? soma zaidi upate siri ya kufanikiwa katika masomo yako katika ngazi tofauti tofauti za elimu ikiwemo elimu ya chuo kikuu.
masomo binafsi kwenye eneo tulivu




KUSOMA MAANA YAKE NINI?



Watu wengi hatujui kusoma maana yake nini,labda hufikiri kusoma ni wakati ule unaposhika daftari au kitabu au kitini kwaajili ya kusomea mtihani ambao unao kesho asubuhi. Lakini watafiti wanasema kusoma hua ni mchakato mpana zaidi ya apo. Kwa kifupi kusoma maana yake hua ni kuandika notsi kwa urefu(kutolea maana kila pointi ulioiandika), kuandika points,bila kusahau kuvisoma hivo ulivoviandika.


NAMNA YAKUFANIKIWA KATIKA MCHAKATO WAKUSOMA:


TAFUTA ENEO LA KIMYA:



inaweza kua chumba tulivu kama hiki ambacho hakina usumbufu kabisa
                   Watu wengi usoma popote bila kujali kama eneo hilo linafaa kwaajili ya kusoma masomo binafsi, wakati wa kusoma ni vema ukatafuta eneoambalo liko kimya na mbali na usumbufu wa namna yoyote kama marafiki wenye kupenda kupiga soga kila wakati au makelele ya magari na muziki
epuka kusikiliza muziki wakati ukiwa eneo la kusoma
na nyingine nyingi. inaweza kua ni maktaba,chumba au eneo lakujificha cha msingi kue kimya,kuna mwanga wakutosha  na kuna hewa yakutosha. Pasi kusahau watu wengi upenda kusoma wakiwa wanasikiliza mziki lakini hii huondoa mawazo yao kutoka kwenye umakini na badala yake huanza
kusikiliza ala za muziki au mashahiri ya nyimbo wanazozisikiliza ni vema ukakwepa kusikiliza mziki wakati wakusoma hii itakusahidia kuongeza umakini wako kwenye jambo unalosoma.







TENGA MDA MAALUMU:


                 Chagua wakati(saa
) maalumu kwaajili ya masomo binafsi na mijadala ya makundi maarufu kama group discussions, chagua siku maalumu kwaajili ya masomo binafsi na mijadala ya makundi (personal studies and group discussions). Tengeneza ratiba na ifuate kwa nidhamu kuu,pamoja na kua na ratiba lakini isikufanye ukose wakati wa mapumziko na kuchangamana na  watu wengine kama ndugu jamaa na marafiki. Hii itakusaidia kuupa nafasi ubongo wako kupumua na kuweza kutunza kumbukumbu vizuri.


KUA NA VIFAA VYOTE KWAAJILI YA KUJISOMEA:


vifaa vyako vyote utakavyo vihitaji hakikisha unavyo
                 Hakikisha unavyovifaa vyote utakavyohitaji wakati wakusoma vifaha hivo ni kama vitabu utakavovisoma,kalamu ya wino,kalamu ya risasi, rula, kifutio daftari yakuandikia point ulizojifunza. kama unasoma mtandaoni kwa kupitia tarakilishi mpakato (laptop) basi hakikisha unajizuia kutumia tovuti zisizohusika kwenye mchakato wako wakusoma, unaweza kutumia program za kuzuia kwa muda utembezi(browsing) wa tovuti zisizohitajika kama kila wakati unapata ushawishi wa kusomaGoogle Chome facebook notification   unaweza kuweka program hii kwenye tarakilishi yako kuongeza umakini na uzuri ni kua itazuia vitembezi vyote kuruhusu utembezi wa tovuti ulizoziuia... Pia zima simu yako ya mkono au iweke kwenye silent mode kuzia usumbufu wowote unaoweza kujitokeza itakua vizuri kama utaiweka sehemu usio weza kuiona kama kwenye begi mpaka utakapo maliza kusoma.
 ujumbe wa facebook au mtandao mwingine kupitia huduma za notifications kwa mfano kwny kitembezi cha


KUA NA FIKRA CHANYA:


             Watu wengi uchukulia kusoma ni kama adhabu ambayo wamepewa na inawalazimu kusoma kwakua hawana njia nyingine ambayo wangeweza kufikia ndoto zao kwa hali hii wengi husoma kwa lengo tu la kufauru mitihani na wakisha faulu mtihani walichojifunza uishia kwenye mtihani. Kwa hali kama hii wengi wao uona ni heri wasome siku moja au usiku mmoja kuamkia kwenye mtihani.. Katika zama hizi hata zile za zamani mtu yeyote ambaye alikua na anasoma kwa lengo la kufauru mtihani basi mtu huyu yuko kwenye hatari kubwa sana. Tumeshuhudia sikuhizi watu wengi wanamaliza vyuo vikuu wakiwa hawajui vema kazi zao na hii hutokana na wengi kutokujua nini haswa walichokua wanajifunza hili limekua tatizo hata wanapoenda kuomba kazi na mabosi wao kuwaona hawana ujuzi wakutosha kuweza kuaminiwa katika kupewa kazi wanazoziomba.. Inampasa kila mtu ambaye ameamua kusoma ajue kwa undani anachosomea na aweze kukielezea na kukitenda kwa ufasaha,wepesi wa kufanya haya utakuja endapo kila mmoja atapenda kile anachojifunza na kuweka bidii kukijua kwa undani. Faida iliopo ni kua hata kama mtu huyu hataajiliwa basi itakua rahisi kwake kubuni njia za kujiajili na kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira mtaani.


USIPENDE KUHARISHA MAMBO:


Kwa lugha ya kingereza tabia hii huitwa "procrastination", hili tatizo ni tatizo ambalo wengi wetu tunalo hasa kwa kazi ambazo zinaonekana kutohitajika hivi karibuni.. Mtu ujikuta anasogeza ratiba mbele ili aweze kuapata mda wakufanya mambo mengine ambayo andhani kua ni ya muhimu kuliko yalioko mbele yake, wanafunzi wengi katika ngazi mbali mbali hupoteza mda mwingi wakipiga soga na marafiki au wakicheza michezo ya video (video games), wengine huenda kwenye mambo yaoya biashara au hata kuzurula wakiamini kua watasoma dakika ya mwisho mtihaniukikaribia madhara ya kuhairisha mambo ni mengi ikiwemo

  • KUA NA MSONGO WA MAWAZO
  • KUTOELEWA UNACHOKISOMA 
  • KURUKA POINT MUHIMU
  • KUTOPATA UJUZI ULIOKUSUDIWA NA WAANDAA MITAALA NA WAAJILI WAKO BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA CHUO
  • UNAWEZA KUSABABISHA UKAFELI MITIHANI HASA UNAPOKUA KWENYE MITIHANI YA MWISHO WA MWAKA 


MALENGO YA MFULULIZO WA MAKALA HIZI NI:

  • Kufanikisha ongezeko la ufauru katika mitihani
  • kuhimiza wanafunzi kujifunza ujuzi unaohitajika na watengeneza mitaala pamoja na waajili baada ya kuhitimu masomo yao
  • kukuza tabia ya uwajibikaji katika kazi na ushirikiano
  • kupunguza misoongo ya mawazo
  • kuhokoa mda kwa kufanya mambo sahihi
  • kutengeneza ratiba maalumu ya masomo
  • njia za kujifunza kwa ujanja na kwa bidii kubwa
 KAA CHONJO KWA MAKALA NYINGINE ZA MASOMO ZITAKAZOKUJA HIVI KARIBUNI.



picha ni kwa msaada wa www.wikihow.com na www.google.com


Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAMNA YA KUTUMIA WI-FI YAKO KUTOKA KWENYE TARAKILISHI (KOMPYUTA)

UTANGULIZI: Habari ndugu wasomaji, leo ntawafundisha namna yakutengeneza Wi-Fi (wireless fidelity) kutoka kwenye tarakilishi mpakato au ya kwenye desk: MAHITAJI: 1.  TARAKILISHI (KOMPYUTA) YA MEZANI(DESKTOP) AU MPAKATO YENYE WIRELESS CARD (KADI YA WIFI) AU YENYE UWEZO WAKUDAKA WIRELESS AU BLUETOOTH 2. UJUZI WA KAWAIDA WA KUTUMIA TARAKILISHI  HATUA YA KWANZA: Unahitajika kua na uwezo wakuunganisha intanet kwenye kompyuta yako kama utatumia modem au utatumia wireless(Wi-Fi) kutoka kwenye eneo ambalo tarakilishi yako imeunganishwa. intanet ya WiFi (kwenye duara jeusi) HATUA YA PILI: Tutatakiwa kushusha (download) Baidu "wifi share app" kutoka kwenye tovuti ya PC FASTER nimekuwekea link hapa uishushe haraka   shusha baidu moja kwa mojahapa    au unaweza tembelea tovuti yako hapa  shusha program yako ya Baidu kwenye tarakilishi yako( kwenye picha ninatumia program ya IDM kushusha BAIDU kwa haraka ) Simika ( install

VYOO VYA KUKAA VINAWEZA KUSABABISHA SARATANI

Habari za leo ndugu wasomaji wa blogu ya Sayansi Leo,katika makala hii ya leo tutazungumzia njia sahihi ya kujisaidia haja kubwa. Ndio njia sahihi yakujisaidia haja kubwa,linaweza onekana kua ni swala la ajabu au la utani lakini mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamekuja na madhara pamoja na faida. kielelezo na.1 Kwakuanza tutatazamia juu ya njia ya asili ambayo binadamu anatakiwa kutumia iwapo ataenda haja kubwa..          Kwa mazoea, jamii nyingi za Afrika watu wake huchuchumaa waendapo haja kubwa. Katika miaka ya hivi karibuni baada ya mapinduzi ya viwanda uko katika nchi za magharibi kumeundwa vyoo vya kukaa. Vyoo hivi vimeonekana kua ni ishara ya maendeleo katika jamii za Wafrika ambao wengi walizoea vyoo vya shimo.. Vyoo hivi sio vyakwanza bali  ni muendelezo wa vyoo vya kigae vyakuchuchumaa vilivoiga mfano wa vyoo vya awali vya asili ambavo pia vilikua vyakuchuchumaa.  vyoo vya vigae vya kuchuchumaa viliboreshwa kwa kuwekewa mfumo wa kujisafisha endapo mtu atamaliza